Tuesday, April 6, 2010

Pendekezo la Kipindi cha “Somafuraju”
Wahusika: Christine Kasiva
Mashirima Kapombe
Portia Opondo

Pendekezo hili ni kulingana na mradi wa mwisho, katika somo la “COM 361A: Audio Production”. Tukizingatia haya, tumekubaliana kufanya kazi kama kikundi cha watu watatu:

Produsa: Portia Opondo.
Mhariri: Mashirima Kapombe.
Muandishi: Christine Kasiva.

Kipindi chetu kinaitwa “SOMAFURAJU”. Neno tulilotunga kutokana na malengo makuu ya kipindi:

Ku-somesha
Ku-furahisha
Ku-julisha

Yaliyomo katika kipindi hiki yatagawanywa katika vipande vinne:

Mambo ya sasa: Hapa tutazingatia mambo yanayotokea katika chuo kama siasa na athari zake kwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Daystar. Tutakuwa na mahojiano ambapo tutawahusisha wanachama wa DUSA (Serikali ya wanafunzi) na wanahabari wa Shine na Involvement kupata maoni yao.
Mitindo na utalii: Hapa tutagusia mitindo ya mavazi, michezo inayomfurahisha mwanafunzi sana katika msimu huu na sehemu za kwenda kupumzika wakati wa likizo fupi au wikendi.
Dondoo: Sehemu hii itashughulikia hadithi za kuchekesha na uvumi/udaku unaoendelea humu chuoni.
Burudani: Msikilizaji atapata kujulishwa visa vinavyotarajiwa kutendeka humu chuoni na pia nje ya chuo.

Manufaa ya “Somafuraju” kwa stesheni ya Shine FM
Kwa kuwa ni kipindi kipya, kitaongezea vipindi katika orodha iliyoko.
Kipindi hiki kitatosheleza mahitaji ya msikilizaji (mwanafunzi wa Daystar), kwa kumsomesha, kumfurahisha na kumjulisha. Aidha kwa njia hii, kitafikia malengo ya stesheni yenyewe.
Kipindi kimejaa dhana mpya, ambazo zitaongezea katika tofauti za vipindi vya Shine.


Manufaa kwa wanakikundi
Itatupatia fursa ya kutumia mafunzo tuliyopata darasani kufanya kazi yenyewe.
Itatuwezesha kupata kionjo cha vile kazi inavyofanywa na watangazaji wengine katika stesheni zengine.
Kwa kuwa ni kipindi cha Kiswahili, kitatuwezesha kunadhifisha msamiati wetu na uzungumzaji wa lugha yenyewe.
Mradi huu utaongezea katika maktaba zetu za kazi tulizofanya tukiwa bado chuoni.

1 comment:

  1. A good idea for a Kiswahili Show. Revise script according to suggestions provided by I and Shine management then post again. Rework your jingle by adding TX day and time. Make it more catchy and upbeat!

    ReplyDelete